Shirika la afya duniani WHO linasema kwa msichana wa umri wa
miaka miwili ambaye alithibitishwa kuwa mgonjwa wa kwanza wa ebola nchini Mali
alisafiri kilomita kadha kwa basi nchini humo huku akionyesha dalili za kuugua
ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 40 ambao walikaribiana naye wametengwa. Huenda
msichana huyo alisafirishwa kwenda nchini Mali na nyanyake baada ya mazishi ya
mamake nchini Guinea moja ya nchi ambazo zimeathirka pakubwa na ugonjwa wa
ebola.
Utawala nchini Mali sasa umethibitisha kuwa msichana huyo
ameaga dunia kwenye hospitali moja mjini Mayes alikokuwa akipewa matibabu.
Mwandishi wa BBC anayehusika na masuala ya afya anasema kuwa
huenda ikawa changamoto kubwa kuwapata watu wengine ambao walikaribiana na
msichana huyo.
No comments:
Post a Comment