Makreti ya soda yalivyoanguka.
Baadhi ya kreti za soda zikiwa zimezagaa eneo la ajali.Mmoja wa wahusika akitoka kuzima na kuuchomoa ufunguo wa gari lililopata ajali.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akilinda usalama eneo hilo.
Askari wa usalama barabarani wakiwa eneo husika.
Sehemu ya foleni inayosababishwa na gari hilo.
WATU watatu akiwemo dereva wa gari la kampuni ya soda ya
Coca Cola walipata michubuko kadhaa katika ajali iliyotokea leo asubuhi maeneo
ya Lugalo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu,
mmoja wa mashuhuda amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari ndogo kuingia
ghafla mbele ya gari hilo kubwa
lililokuwa limebeba vinywaji na ndipo
gari kubwa likiwa katika kukwepa likajikuta likianguka ubavu.
(Habari/Picha na: Gabriel Ng’osha/GPL)
No comments:
Post a Comment