Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu
anazodaiwa kutenda baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.Mahakama hiyo inasama kuwa
Kenyatta alihusia katika kupanga na kufadhili ghasia za kikabila baada ya
uchaguzi uliozua utata mwaka 2007/08Zaidi ya wakenya 1,000 waliuawa kwenye
gasia hizo.
Ruto ambaye ni rais kwa muda naye pia anakabiliwa na kesi
katika mahakama hiyo ya ICC
Mawakili wa Kenyatta wanasema kuwa kesi hiyo inapaswa
kufutiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.
Kenyatta ameombwa na mahakama hiyo kufika
mbele yake ili
kujadili malalamiko yaliyowasilishwa na kiongozi wa mashtaka Fatou Bensouda
kwamba serikali ya Kenya imekataa kuwasilisha ushahidi unaohitajika katika kesi
ya Kenyatta. Majaji wa mahakama hiyo hata hivyo watathmini kauli kutoka kwa
pande zote mbili.
Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa pia kutangaza tarehe
ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Kenyatta.
ICC imemtaka Kenyatta kujibu madai ya upande wa mashitaka
kuwa Kenya inakataa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.
Rais Kenyatta akikagua gwaride la heshima kabla ya kuondoka
nchini kuelekea Hague
Mwezi Septemba, mahakama iliahirisha kesi dhidi ya Kenyatta
baada ya upande wa mashitaka kusema kuwa Kenya imekosa kutoa ushahidi
unaotakikana na mahakama hiyo.
Mashahidi wa upande wa mashitaka wamejiondoa katika kesi
hiyo.
Mamia ya wabunge wa Kenya wanatarajiwa kuambatana na
Kenyatta kama ishara ya kumuunga mkono.CHANZO BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment