Mashindano ya kukamua maziwa mwaka huu yameleta wasiwasi wa
baadhi ya washiriki kutumia dawa za kuongeza nguvu. Michuano ya dunia
iliyofanyika nchini Italy, imeshuhudia bingwa akikamua lita 8.7 katika kipindi
cha dakika mbili. Mshindi alikuwa Gianmario Ghirardi na ng'ombe wake Mirka.
Hata hivyo washindi watatu wa juu mwaka huu wamekabiliwa na tuhuma za matumizi
ya dawa za kuongeza nguvu baada ya washindi hao wote
kukamua maziwa zaidi ya
lita saba katika kipindi cha dakika mbili. Kwa mujibu wa tovuti ya i100, bingwa
wa mwaka 2013 Maurizio Paschetta amesema: "Kwa mashindano makiubwa kama
haya, ungetegemea vipimo vya matumizi ya dawa kufanyika kwa ng'ombe na hata
wakamuaji, ili kuwepo na hakikisho la uwazi katika nafasi za juu."
Hata hivyo msaidizi wa rais wa shirikisho lililoandaa
michuano hiyo amesema; "Tuliwapima ngombe wote kwa muda wa saa moja,
halafu pia kuna majaji wanane."
No comments:
Post a Comment