Kijana Zakayo Leonard (26) akitumikia adhabu ya viboko 120.
SHERIA iliyopitishwa na wakazi wa Arumeru mkoani Arusha ya
kuwachapa viboko 70 hadi 120 wasichana wanaovaa nusu uchi na wavulana wanaovaa
mlegezo, kuvuta bangi, wizi, matusi na ulevi nyakati za kazi imeanza kufanya
kazi baada ya kijana Zakayo Leonard (26) kuchapwa viboko 120 kwa makosa
mbalimbali likiwemo uchafu wa kutofua nguo zake.
Kijana huyo mkazi wa Ilboru, alihukumiwa adhabu hiyo kwa
kuchapwa viboko 70 akidaiwa kutenda kosa
la kumshambulia baba yake mzazi aliyetambulika kwa jina la mzee Ng’uraa na
kumng’oa jino moja.
Pia alitandikwa viboko 30 kwa kosa la kumtolea maneno machafu
mzee wa kimila (Laigwanani) na baadaye alicharazwa viboko 20 kutokana na tabia
ya uchafu wa kutofua nguo zake.
Hata hivyo, mara baada ya adhabu hiyo ya viboko 120 kwa
mkupuo, kijana huyo alizimia na kushindwa kuinuka wala kutembea hali
iliyolazimika kusaidiwa kwa kubebwa na morani wa Kimasai hadi nyumbani kwake.
Zoezi la kumsurubu kijana huyo likiendelea.
Adhabu hiyo
ilitekelezwa hadharani mbele ya wazee wawili wa ukoo (Laigwanani) waliokuwa wakishuhudia
huku mtuhumiwa akitakiwa kutojigusa popote wakati wa utekelezaji wa adhabu hiyo
na kwamba iwapo
angejishika popote viboko hivyo alivyochapwa vingefutwa na
kurejea upya. Wazee wa makabila ya Wamasi, Waarusha na Wameru wamejiwekea
utaratibu wa kimila bila kujali kama unafuata maadili ya mwanadamu kwa
kuwaadhibu wahalifu hadharani bila kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.chanzo Gpl
No comments:
Post a Comment