WAJUKUU wa marehemu Sabina Ngalu (77) wameibua kutuko
makaburini kufuatia kuzama ndani ya kaburi la marehemu huyo na kugoma kutoka
wakidai kwamba mpaka walipwe shilingi laki moja (100,000), Uwazi lina mkanda
mzima.
Wajukuu wa bibi huyo wakiwa kaburini. Tukio hilo la aina
yake lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kitongoji cha Nyamwanza Kata
ya Sima wilayani Sengerema mkoani Mwanza muda mfupi baada ya mwili wa marehemu
kuwasili eneo la mazishi kwenye shamba lake ukitokea Kanisa la Roman Katoliki
Parokia ya Yesu Kristo Mfalme la mjini Sengerema.
Sababu za wajukuu hao kung’ang’ania ndani ya kaburi hilo
walitaka wapewe ng’ombe mmoja au pesa hizo taslimu kwa mjibu wa mila na desturi
za kabila la Kisukuma jambo ambalo lilipingwa na baadhi ya wanandugu waliodai
mila hizo zilipitwa na wakati.
Kufuatia wajukuu hao kuendelea kugomea ndani ya kaburi, kaka
wa marehemu, Enosi Ngalu alikwenda kukata fimbo na kuwashukia kisha kuwacharaza
viboko wote huku nao wakisisitiza hawatoki mpamka ‘kieleweke’.
Padri na wananchi wakiwa makaburini. Baadhi ya wajukuu
walioonja joto la jiwe ya kuchapwa viboko ni Andrea Mabula, Sabina Bukuru,
Johari Bukuru, Asha Bukuru, Faida Bukuru, Yuves Petro, Semeni na kiongozi wao,
Enos Ntilaga. Kitendo cha wajukuu hao
kuendelea kugoma kutoka kaburini
kilimchefua Padri Nicodemus Mayalla ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Yesu
Kristo Mfalme, Sengerema ambaye aliamua kuondoka eneo la maziko huku
akiwataarifu polisi kuhusiana na vurugu hizo.
Kufuatia hali hiyo, mmoja wa waombolezaji alizama mfukoni na
kutoa kiasi hicho cha pesa na kuwapa ndipo walipokubali kutoka dani ya kaburi
hilo ili mazishi yaendelee. Ili kuonesha alikerwa na kitendo hicho, Padri
Mayalla ambaye kwa wakati huo alikuwa amewekwa chini na baadhi ya ndugu
wakimsihi kutosusia mazishi hayo, aligoma kurejea kaburini kuongoza ibada ya
mazishi.
Jeneza lenye mwili wa bibi huyo likishushwa kaburini. Baada
ya vuta nikuvute, hatimaye Padri Mayalla alikubali kuendelea na ibada lakini
aliwataka wajukuu hao kurudisha pesa waliyochukua na kuwaomba radhi wana mtaa
huo na ndipo yeye aweze kurudi kaburini. Wajukuu hao waliitwa mbele ya padri
huyo na mbele ya wana mtaa, wakaomba samahani ikiwa ni pamoja na kurudisha
kitita hicho cha pesa paroko huyo naye akarejea kaburini na kuongoza ibada ya
mazishi.
Hata hivyo, wakati ibada ikiendelea polisi zaidi ya wanne
kutoka Kituo cha Polisi Sengerema wakiwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun
(SMG) na mabomu ya machozi walifika eneo la tukio ili kuhakikisha amani na
utulivu vinatawala.
Polisi akiwa eneo la tukio. Cha kushangaza, saa baada ya
kutoka makaburini, wajukuu hao waliwahi nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Mlimani,
Kata ya Nyatukala wilayani Sengerema na kuanzisha timbwili jingine kwa kuficha
chakula na vyombo vya kupakulia wakidai warudishiwe pesa yao waliyoirejesha
makaburini kwa shinikizo la baba paroko.
Baada ya timbwili hilo kukolea, mmoja wa wafiwa alizama
mfukoni na kutoa shilingi laki moja na kuwakabidhi wajukuu hao ambao
walirudisha chakula jikoni na taratibu za waombolezaji kupata chakula
ziliendelea.
No comments:
Post a Comment