Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, October 20, 2014

TAZAMA VIDEO YA MTI ULIOANGUKA NA KUINUKA BAADA YA MIAKA 3 HUKO TABORA

Pichani ni mti unaodaiwa kunyanyuka ghafla baada ya kuanguka miaka mitatu iliyopitakatika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma ,ambapo wilaya ya Uyuwi mkoani Tabora.
Katika hali ya kushangaza huku kila mtu akifikiria yake baaya ya juzi huko mkoani Tabora, kutokea tukio la aina yake ambapo inaelezwa kuwa mti aina ya Msufi uliokuwa umeanguka yapata miaka mitatu iliyopita umesimama ghafla tena kwa sauti kubwa ya mrindimo na kuwafanya wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo.



Tukio hilo limetokea Oktoba 17,mwaka huu,katika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma katika wilaya ya Uyuwi mkoani Tabora.



Inaelezwa kuwa mti huo wenye kipenyo cha futi 2 uliinuka na kuwa 



kama zamani baada ya kutokea upepo mkali katika kijiji hicho.

Wananchi walikusanyika kila mmoja akitaka kuchukua angalau gome la mti huo kwa ajili ya dawa ama kumbukumbu , na haya ndio maajabu ya Tanzania. 

No comments:

Post a Comment