Mtu
mmoja anasemekana kupoteza maisha na mwingine kujeruhiwa baada ya
Magari Mawili waliyokuwa wanaendesha kugongana uso kwa uso katika eneo
la Trans Oil kata ya Nyasubi Wilayani Kahama mkoani Shinyanga usiku huu.
Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku huu likihusisha
gari aina ya Coster mali ya Kampuni ya CK Safari Tours yenye namba
T-468-CAL kugongana na Semi Teller aina ya Scania yenye namba T-498-BVH.
Kwa mujibu wa Mashuhuda,
gari aina ya Coster ilikuwa ikitokea eneo la kituo cha Mafuta kwenda
Phantom, huku Scania hiyo ikitokea jijini Dar-es-salaam kwenda nchi
jirani na ndipo zikagongana uso kwa uso.
Taarifa zinasema Dereva
wa Scania hiyo ndiye huenda amefariki dunia huku dereva wa Coster hiyo
akisemekana kujeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama
kwa matibabu.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, na
tayari Jeshi la polisi wilayani Kahama limefika katika eneo la tukio na
taratibu za kuyatoa magari hayo katikati ya barabara zinaendelea.
CREDITS KWA DUNIA KIGANJANI
No comments:
Post a Comment