Dk. RK Gupta aliyetiwa mbaroni.
DAKTARI anayehusishwa na tukio la vifo vya watu
13 katika kituo cha kutoa huduma ya kuzuia uzazi kwa njia ya upasuaji jimboni
Chattisgarh nchini India, Dk. RK Gupta ametiwa mbaroni
Baadhi ya akina mama waliofanyiwa upasuaji wakiwa hospitali.
Dk Gupta na msaidizi wake waliwafanyia upasuaji wananawake
83 katika kijiji cha Pendari ndani ya saa 3 Jumamosi iliyopita na kusababisha
vifo 13 huku wengi wakiwa wamelazwa hospitali, 20 kati yao wakiwa katika hali
mbaya.
Ram Avtar aliyempoteza mke wake aitwaye, Nem
Bai akiomboleza na wanaye huko Bilaspur, Chattisgarh.
Serikali nchini humo inamtaka daktari mmoja kutoa huduma ya
upasuaji kwa watu 35 tu kwa siku.
Ndugu na jamaa wakiomboleza kifo cha mama mmoja aliyefariki
baada ya upasuaji huo.
Maandamano yamefanyika baada ya tukio hilo la vifo, huku
serikali ya Jimbo la Chhattisgarh ikitoa amri ya kufanyika kwa uchunguzi.
No comments:
Post a Comment