BEYONCE 'ATESA' KWA KIPATO
Akiingiza zaidi ya dola milioni 115, Beyonce amekuwa
mwanamke anayelipwa zaidi katika muziki mwaka huu. Alikuwa na "mwaka wenye
mafanikio zaidi", akifanya maonesho 95 na kuingiza wastani wa dola milioni
2.4 katika kila jiji, kwa mujibu wa Forbes. Mikataba na makampuni kama vile
Pepsi na H&M, pamoja album iliyotolewa 'ghafla' Disemba 2013,
zimemsaidia
kushika nafasi hiyo. Albam hiyo ilitolewa kwenye iTunes bila hata kufanyiwa
matangazo ya utambulisho. Beyonce ametangaza pia kuwa atatoa album baadaye
mwezi ujao, itakayokuwa na nyimbo mpya na video ya tamasha.
Taylor Swift ameshika nafasi ya pili katika orodha hiyo ya
Forbes, akiingiza takriban dola milioni 64. Nafasi ya tatu imechukuliwa na
Pink, aliyefanya matamasha 85 katika kipindi ambacho Forbes ilikuwa ikifanya
tathmini yake. Alikadiriwa kuingiza dola milioni 52. Wasanii wengine katika
orodha hiyo ni Rihanna katika nafasi ya nne akiingiza dola milioni 48 na Katy
Perry katika nafasi ya tano aliyetengeneza dola milioni 40. Forbes ilipiga
hesabu zake kwa kutazama mapato kutokana na "matamasha, mauzo ya rekodi,
mauzo ya bidhaa za kimuziki, mikataba ya makampuni ya kibiashara na
mengineyo" kati ya Juni 2013 na Juni 2014. Baadhi ya wasanii maarufu ambao
walikosa nafasi za juu ni pamoja na Madonna, Nicki Minaj na Alicia Keys.
Orodha ya kumi bora:
1: Beyonce - Dola 115m
2: Taylor Swift - Dola 64m
3: Pink - Dola 52m
4: Rihanna - Dola 48m
5: Katy Perry - Dola 40m
6: Jennifer Lopez - Dola 37m
7: Miley Cyrus - Dola 36m
7: Celine Dion - Dola 36m
9: Lady Gaga - Dola 33m
10: Britney Spears - Dola 20m
Chanzo: Forbes/BBC
No comments:
Post a Comment