Vyombo vya habari vya Serikali nchini Zimbabwe vinaripoti
kuwa Makamu wa Rais,Joyce Mujuru, ameondolewa kwenye kamati kuu ya chama cha
ZANU-PF.
Mujuru anashutumiwa kupanga mauaji dhidi ya Rais wa nchi
hiyo,Robert Mugabe.
Hatua hiyo imekuja baada ya Kampeni dhidi ya Mujuru
iliyofanywa na Mke wa Rais Mugabe, Grace ambaye kwa kiasi kikubwa anaamini
anataka kumrithi Mumewe atakapotoka madarakani.
Viongozi kadhaa wa ZANU-PF wameshindwa kutetea nafasi zao
katika Chama hicho.
Bi Mujuru alitarajiwa kumrithi rais Mugabe mwenye umri wa
miaka tisini.
Kamati ya uchaguzi katika mkoa wa kaskazini wa Mashonaland
ya kati imekataa wasifu wa Makamu wa rais nchi hiyo Joice Mujuru kama baadhi ya
stakabadhi zake za kuomba kazi katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumanne.
Bi Mujuru ambae alikuwa mmoja wa viongozi wenye ushawishi
mkubwa katika chama tawala cha ZANU PF, alikuwa pia waziri mchanga zaidi katika
baraza la mawaziri la rais Robert Mugabe wakati taifa hilo lilipojinyakulia
uhuru wake mwaka wa 1980.
Alipanda ngazi na kuwa kiongozi wa pili mwenye ushawishi
zaidi chamani kutokana na wasifu wake wakati wa vita vya uhuru dhidi ya utawala
wa kikoloni wa Uingereza.
Katika kipindi cha miezi michache iliyopita - amekuwa akishambuliwa
katika mikutano ya kampeni kutoka kwa mke wa rais Robert Mugabe, Grace, ambaye
anamhutumu kwa kutowajibika, ufisadi na amemtaka ajiuzulu.
Kumekuwa na fununu kuwa Bi. Mugabe amekuwa na nia na ari ya
kutaka kumrithi mumewe.
Mmoja wa wapinzani wakuu wa Mujuru, ni Waziri wa Sheria
Emmerson Mnangagwa, na inaaminika kuwa ni mmoja wa wagombea wakuu ambao
wanaongoza katika harakati za kumrithi rais Mugabe ambaye anatimu miaka 91
miezi mitatu ijayo.
Haijabainika ikiwa Mujuru atahudhuria kongamano la uchaguzi
wa chama cha ZANU PF wiki ijayo, ambapo uongozi mpya wa chama hicho utateuliwa
No comments:
Post a Comment