Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 27, 2014

WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA KUWA MGENI RASMI KWENYE UZINDUZI WA ALBAMU ‘USILIE’ DESEMBA 7, 2014

 Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto (kulia). Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Na Mwandishi Wetu.
WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda ametajwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ‘Usilie’ ambayo itapatikana kwenye DVD Desemba 7, mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto, alisema hafla hiyo itafanyika kwenye Ukumbi wa PTA uliopo Uwanja wa Sabasaba, Dar es Salaam.
Mbali ya uzinduzi huo Misheto alisema pia wasanii mbalimbali wa filamu watanogesha siku hiyo.


 Aliwataja waimbaji wa injili ambao watakuwepo siku hiyo kuwa ni Leah Mudy, AIC (T) Vijana Chang’ombe, Accasia Singers, Papson Mastaki kutoka Kenya na Frank Hume kutoka Boston nchini Marekani watatumbuiza.
Uzinduzi huu umeratibiwa na Misheto Promotion, ambapo kabla ya uzinduzi huo kutafanyika huduma za bila malipo za kiafya na kitabibu kutoka kwa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, ambayo yamekuwa yakiikabili jamii.
Misheto ameyataja magonjwa hayo kuwa ni moyo, figo, kisukari na mengineyo ambapo huduma hiyo itatolewa na madaktari bingwa nchini.
“Huduma hii itaanza saa mbili asubuhi na itatolewa bure, ikiwemo ushauri na kwa wale ambao wataweza kutibika watatibiwa, ila ambao watakuwa kesi zao zimekuwa ni kubwa zaidi watapewa ushauri wa bure wa kuendelea na matibabu katika hospitali kubwa na hakutakuwa na kiingilio," alisema Misheto.

No comments:

Post a Comment