“.. Kutokana na Serikali kudaiwa bilioni 102 na bohari ya
madawa MSD hali ya Hospitali zetu ni mbaya sana.. wagonjwa wanaendelea kuteseka na maradhi,
madawa hamna.. wanawake wanakufa, watoto wanateseka.. huku sisi waheshimiwa
wabunge tukiendelea kukaa humu tukila viyoyozi’
‘kwa taarifa tulizonazo Mheshimiwa Rais yupo nje
kaenda
kuchekiwa afya yake.. Ili tuwatendee haki Watanzania waliotuweka katika bunge
hili na tuweze kuokoa maisha yao naomba bunge lako liahirishe shughuli
zinazoendelea tuweze kujadii jambo hili kwanza.. tulipatie ufumbuzi kwa maslahi
ya Watanzania.. na kwa maana hiyo naomba kutoa hoja na waheshimiwa wabunge
naomba mniunge mkono..” – Rukia Ramadhani, mbunge viti maalum CUF.
Mbunge Ally Kessy akajibu hoja hiyo;- “..Wabunge wangapi wa
upinzani tayari wameshawahi kwenda India mara sita.. Kwa majina nawajua tena wa
CUF wamekwenda India kutibiwa mara tatu mara nne leo mnazungumzia habari ya
Rais kwenda kutibiwa Marekani, aende kutibiwa wapi Zanzibar? Acheni mambo yenu
hayo..”
Naibu Spika wa Bunge akafunga mjadala huo;- “..Waheshimiwa
wabunge ningewaomba sana kuhusiana na masuala ya wagonjwa wetu mbalimbali wawe
ni wabunge.. Awe ni mheshimiwa Rais na wanatibiwa wapi.. Naliomba jambo hili
tuliache litatuharibia hali ya hewa bila sababu jamani.. Nawaombeni sana hilo
nimelitoa katika utaratibu na kwenye hansard tulifute jamani..”- Job Ndugai
No comments:
Post a Comment