MTANGAZAJI wa zamani wa Redio Clouds FM ambaye sasa ni
ripota wa Redio Deutsche Welle ya Ujerumani, George Njogopa ameporwa gari usiku
wa kuamkia Jumatatu iliyopita maeneo ya Maryland Bar, Mwenge jijini
Dar.Mtangazaji wa zamani wa Redio Clouds FM ambaye sasa ni ripota wa Redio
Deutsche Welle ya Ujerumani, George Njogopa akiwa Rais Jakaya Kikwete.
Kwa mujibu wa chanzo, mtangazaji huyo alikuwa na mwanamke
ambaye anadaiwa kuhusishwa kuongoza tukio zima la wizi huo wa gari aina ya
Spacio New Model lakini mwenyewe amekanusha.” Sikuwa na mwanamke, walionipora
walinivamia na kunitupa maeneo ya Maryland, tayari nimeshafungua jalada katika
Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa uchunguzi zaidi,” alisema Njogopa.
CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment