Mke wa Gardner G Habash, Judith Wambura Mbibo, ‘Lady Jaydee’ akipozi.
Prizenta aliyetua Radio E-FM hivi karibuni akitokea Radio Times FM, Gardner G Habash ‘Kapteini’ anadaiwa kumpandisha kortini mkewe, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kisa kikisemekana ni mgawanyo wa mali hivyo anataka haki yake baada ya kuwepo kwa madai mazito ya ndoa yao kuvunjika.Kwa mujibu wa madai hayo, inasemekana kwamba Gardner amekimbilia
mahakamani akidai apewe talaka na waweze kugawana mali walizochuma wote
ili kila mmoja achukue hamsini zake.
Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa familia hiyo kililiambia
gazeti hili kwamba, siku chache baada ya kutengana na huku hali ikizidi
kuwa mbaya, mtangazaji huyo alichukua hatua ya kutafuta msaada kwa
wanasheria.
“Msinitaje jina ila ninachowaambia ni kwamba Gardner tayari ameshampata mwanasheria anataka kumshitaki Jaydee.
“Msinitaje jina ila ninachowaambia ni kwamba Gardner tayari ameshampata mwanasheria anataka kumshitaki Jaydee.
“Anachohitaji ni kugawana mali zao, kila
mtu afanye maisha yake na ukiangalia tu Gardner hana mpango tena wa
kuendelea na maisha ya ndoa na Jaydee ila Jide yeye bado ana matumaini
ya kurudiana wawe pamoja na hasa kinachomuuma ni kugawana mali.
Prizenta aliyetua Radio E-FM hivi karibuni Gardner G Habash ‘Kapteini’ Lady Jaydee
“Yaani Gardner ameshafanya kila aina ya jitihada ya kutaka waachane
kiroho safi lakini Jaydee anaonekana kutokubaliana na wazo hilo kwani
anaogopa ule usemi kwamba mwanamke mjinga huvunja ndoa yake kwa mikono
yake mwenyewe,” kilisema chanzo hicho na
kuongeza:“Ishu ya kugawana mali ya Gardner na Jide ndiyo habari ya mjini na ili jamaa apate chake ameona heri atafute mkono wa sheria.”
kuongeza:“Ishu ya kugawana mali ya Gardner na Jide ndiyo habari ya mjini na ili jamaa apate chake ameona heri atafute mkono wa sheria.”
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu’ kwamba, kitendo cha Jaydee
kutangaza kubadili mwelekeo wa mali zake akianza kwa kubadili jina la
ule mgahawa wake kutoka lile la Nyumbani Lounge na kuuita M.O.G ndicho
kimemshtua Gardner na watu wake wa karibu.
Kilendelea kudai kwamba, pia ishu ya Jaydee kubadili jina la Bendi ya
Machozi na kuiita Lady Jaydee and the Band, nayo imemchochea Gardner na
kuamua kukimbilia mahakamani. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti
hili lilimtafuta Gardner ili aweke wazi madai ya kutaka kumburuza
mahakamani mkewe huyo na haya ndiyo majibu yake mafupi: “Kaka kusema
kweli hiyo ishu nashindwa kuizungumzia maana hata sijui wewe umeipata
wapi dah.”
Gardner na Jaydee ambao walifunga ndoa mwaka 2005, wamekuwa wakidaiwa
kuwa hawapo pamoja tena huku majukumu ya mtangazaji huyo ambaye alikuwa
meneja wa mwanamuziki huyo yakichukuliwa na ndugu wa Jide ambaye ni
msanii wa Bongo Fleva aitwaye Wakazi.
No comments:
Post a Comment