Rais wa nchi ya China, Xi Jinping akiwapa mkono wananchi wa
Tanzania.
Inadaiwa kuwa wanunuzi, raia wa Uchina walinunua maelfu ya
kilo za pembe za ndovu nchini Tanzania na kuzitorosha kutoka nchini humo katika
ndege ya binafsi ya Rais wa Uchina, Xi Jinping wakati alipozuru bara Afrika.
Kulingana na shirika la ujasusi la mazingira lililo na makao yake mjini London.
Ndege ya rais wa China.
Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja tu kabla ya ziara ya rais
huyo wa China kuja nchini tanzania mwaka ulioipita ambapo zilifichwa katika
mifuko ya wanadiplomasia ili kutokamatwa.
Shirika hilo pia linadai kwamba wajumbe waliokuwa
wakiandamana na Rais Xi walinunua viwango vikubwa vya pembe hizo.
Uuzaji wa Pembe za ndovu ulipigwa marufuku mwaka 1989 ili
kuwazuia wawindaji haramu kuwaua ndovu.
(CREDIT: BBC SWAHILI)
No comments:
Post a Comment