Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, November 7, 2014

VILIO NA HUZUNI:WATU 12 WAMEFARIKI DUNIA IFAKARA, BAADA YA BASI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGA TRENI

 Basi la Super Aljabir baada ya ajali.
 watu 12 wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa baada ya Basi la Super Aljabir linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mahenge mkoani Morogoro kugongana na treni maeneo ya Kiberege karibu na Ifakara, Morogoro jioni hii.Ajali hiyo imetokea wakati basi hilo likijaribu kuwahi kuvuka reli kabla ya treni kupita.
Baadhi ya miili katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio.

WATU 12 wamefariki dunia papo hapo na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya basi walililkuwa wakisafiria la Kampuni ya Aljabir kugonga treni eneo la Kiberege Ifakara Wilaya ya Kilombero.


 Kamanda wa polisi mkoani hapa Leonald Paulo alisema  ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 9:15 alasili baada ya basi hilo lilokuwa likitokea Morogoro- Ifakara kugonga Treni ya Tazara iliyokuwa ikitokea Mbeya – jijini Dar es Salaam.
 Kamanda huyo  alisema kati ya watu hao sita wanaume, wanne wanawake na  wawili ni watoto wakike wenye umri kati ya miaka mitano na sita.
Kamanda Paulo aliwataja marehemu watatu waliotambulika katika ajali hiyo kuwa ni Frugensia Lusangila (60), Albeta Lusangila (62) wakazi wa Ichonde Mangula na Joseph Kazwila (34) mkazi wa jijini Dar es Salaam.

 Kamanda Paulo alisema chanzo cha ajali hiyo ni  dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T725 ATD Scania, alivuka barabara yenye makutano na reli bila ya kuchukua tahadhani na hivyo kuigonga treni.

Alisema kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya mtakatifu Fransis Ifakara na kituo cha afya Kibaoni kwa ajili ya matibabu.
Kamanda Paulo alisema  miili ya marehemu nayo imehifadhiwa katika hospitali ya mtakatifu Frances Ifakara.

Alisema dereva wa basi hilo alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea na polisi wanamtafuta wakati uchunguzi ukiwa bado unaendelea.

No comments:

Post a Comment