Watoto
wawili wa kiume wameishtaki Serikali na shirika la ndege la Malaysia
kutokana na kumpoteza baba yao katika ndege ya Malaysia Airlines 370.
Watoto
hao Jee Kinson mwenye miaka 13, na Jee Kinland wameorodhesha majina ya
shirika hilo la ndege, maafisa wa idara ya usalama wa anga na uhamiaji,
na mkuu wa kikosi cha jeshi la anga kuwa wamehusika moja kwa moja na
upotevu wa ndege hiyo mwezi Machi 8 mwaka huu.
Baba
wa watoto hao alikuwa mmoja wa abiria ndani ya ndege hiyo akitokea
Kuala Lumpur Malaysia kuelekea Beijing China, tangu imepotea zimepita
siku 237 na jitihada za kuitafuta bado zinaendelea.
No comments:
Post a Comment