Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, December 23, 2014

ALICHOANDIKA ZITTO KABWE KUHUSU RAIS KIKWETE

"Jakaya Kikwete anaingia ameingia katika mwaka wake wa mwisho wa uongozi wake akiwa na mtihani mkubwa unaohusu ‘legacy’ yake mwenyewe. Ni Kiongozi pekee wa Tanzania aliyeruhusu taasisi za Uwajibikaji kufanya kazi zake na hata yeye kujikuta akichukua hatua kulingana na maamuzi ya taasisi hizo. Kabla yake, hakuna Rais wa Tanzania aliyetoa nafasi kwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya kazi zake kwa uwazi na umahiri. Hatua yake ya kujadili kwa uwazi taarifa ya CAG ya mwaka unaoishia Juni 30, 2006 kwa kuwaita Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, 


kasha Makatibu Wakuu, Ma RAS na Ma DED ilijenga msingi mkubwa wa taarifa zinazofuata za CAG. Mwaka 2012 alifukuza kazi mawaziri 6 na manaibu mawaziri 2 kufuatia Taarifa za Kamati za Bunge za Mahesabu zilizotokana na Taarifa ya CAG.
Haikupata kutokea katika historia ya nchi yetu Rais kufanya hivyo. Hata hivyo, Rais Kikwete amepata changamoto kubwa inayotokana na mafanikio yake ya miaka 9 ya uongozi wake. Namna atakavyo shughulikia suala la akaunti ya Tegeta Escrow, ama itafuta ‘legacy’ yake au itaiimarisha. Akiimarisha atakuwa ‘redefining leader’ – Kiongozi ambaye anatoa changamoto kwenye mazoea na kufanya yale ambayo wenzake walishindwa."

Soma RaiaTanzania kesho Jumatatu katika jarida la Elimu. Hiki ni kitabu changu cha mwisho wa mwaka huu 2014 The Myth of The Strong Leader by Prof. Archie Brown

No comments:

Post a Comment