Garry Neville enzi zake akichezea Manchester United
Mchezaji wa zamani wa Manchester United Gary Neville amesema
kuwa mchuano kati ya timu yake ya jadi na Liverpool hapo Jumapili
inalinganishwa na mchezo kati ya "Mbwa au Bata na Simba Mwekundu".
Neville, wakati alipokuwa akifanya kazi na Sky Sports
alifananisha mchuano huo na mchezo wa baa.
Na pia alisema kuwa Machester United waliponea kushindwa na
Southampton kwa kuibuka washindi kwa 2 -1 jumatatu.
"anaweza kusema atakavyo kwani ni mkongwe lakini
kama
mkongwe inafaa aelewe yale anayosema" Loius Van Gaal alisema "lazima
atilie manane yake maanani"
Lakini Neville amekanusha kuwepo kwa mvutano kati yake na
Van Gaal
Robin van Persie aliifungia Manchester United mabao yote
mawili katika ushindi wao dhidi ya manchester United
Neviile aliulizwa kwenye mtandao wa Twitter kama kuna
mvurugano kati yake na Van Gaal na alisema "mvurugano upi? ambao umebuniwa
na haupo"
Van Gaal alikiri kwamba timu yake ilikuwa na bahati nasibu
kuishinda Southampton kwani pia wameweza kushinda mechi tano mfululizo.
Ushindi huo uliwezesha Manchester United kupanda hadi nafasi
ya tatu
No comments:
Post a Comment