Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, December 31, 2014

PICHA ZINATISHA::MTUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA APIGWA RISASI KATIKA HARAKATI ZA KUTAKA KUTOROKA MAHAKAMANI

Mtuhumiwa wa madawa ya kulevya raia wa Sierra Leone akiwa amepigwa risasi baada ya kutaka kuwatoroka askari magereza katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

 Mtuhumiwa wa Madawa ya kulevya amepigwa risasi na kufa papo hapo kufuatia kutaka kutoroka Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Huyo mshitakiwa ni raia wa Sierra Leone na aliletwa Mahakamani kusomewa shitaka linalomkabili. Akaomba apelekwe msalani mara moja. Alipokuwa msalani akamsoma yule askari alokuwa anamsubiria nje na kuona kazubaa ndipo akaruka ukuta na kutoka nje na kuanza kukimbia. Mtuhumiwa alikuwa kavaa 'Jeans' akaivua kuona inamsumbua. 




Akakimbia akitaka kutokea katika lango kuu la Mahakama ya Kisutu lakini likafungwa haraka. Ndipo akaamua aende akaruke uzio wa pembeni ambao una vyuma vyenye ncha kali".
Wakati huo wote askari walikuwa wanamfukuza kwa nguvu lakini hawakuweza kupiga risasi kwa sababu alikuwa mjanja sana akawa anakimbia katikati ya watu." "Ndipo alipofika kwenye hiyo fensi akijaribu kuruka askari akapiga risasi mbili hewani, jamaa hakutii. Ndipo akaiga risasi moja ikampata mkononi na nyingine mzima kampata shingoni na kufariki papo hapo."

No comments:

Post a Comment