Mmoja wa majeruhi, Mwanahawa Ramadhani, akiwa katika
Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza kupatiwa matibabu baada ya kuvunjika mkono
kutokana na ajali ya gari wakitokea Bagamoyo mkoani Pwani kusherehekea Maulid.
Watu 10 wamejeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Noah
kupinduka katika kijiji cha Kitumbi Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Ajali hiyoilitokea juzi gari hilo likiwa limebeba abiria
wanawake watupu waliokuwa wakitoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kusherehekea
sikukuu ya Maulid kuelekea kijiji cha Kwakibuyu kata ya Songa wilayani Muheza.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Frasser
Kashai, abiria waliopata ajali hiyo walikuwa wakitoka katika Msikiti wa Songa
kwa Kibuyu
wilayani Muheza.
"Walikodi magari mawili yote aina ya Noah moja
liliwabeba wanaume na lingine wanawake kwa ajili ya kuwapeleka Wilaya ya
Bagamoyo mkoani Pwani kusherehekea Maulid," alifafanua Kamanda Kashai.
Alifafanua kuwa baada ya Maulid kumalizika, waligeuza siku
iliyofuata kurejea Muheza.
Alisema kuwa gari iliyokuwa imewabeba wanawake, ilitangulia
mbele na kufuatiwa ya wanaume.
Hata hivyo, Kamanda Kashai alisema walipofika maeneo ya
kijiji cha Kitumbi, gari lililokuwa limewabeba wanawake, lilipinduka na
kusababisha majeruhi hao.
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni baada ya dereva kutaka
kulipita gari lingine ambapo lilitokea gari lingine mbele yake na alipojaribu
kulikwepa, likapinduka
Baadhi ya majeruhi walivunjika mikono katika ajali hiyo.
Na katika hatua nyingine, majeruhi sita wa ajali ya ajali ya
basi dogo aina ya Hiace wakati wakitokea kijiji cha Misozwe kuelekea mjini
Muheza mjini, wamelazwa Hospitali Teule Muheza, wametoa kilio kwa Mkuu wa
Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu, wakidai kwamba tangu wapate ajali hiyo zaidi ya
wiki moja sasa, hawajapatiwa huduma yoyote ya matibabu.
Kutokana na kilio cha majeruhi hao, Mgalu amewaagiza
viongozi wa hospitali hiyo kuwashughulikia haraka majeruhi hao ikiwamo na
kuwapiga picha za X-ray.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya, ameahidi kwamba atafika
hospitali hapo kila siku kusikiliza kero za majeruhi hao.
No comments:
Post a Comment