Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, January 16, 2015

Afya Leo::Usingizi wa Kutosha ni nguvu ya kufanya kazi vizuri mchana


Kila inapofika usiku, watu wengi huuchukulia ni wakati wa kupumzika. Siyo kupumzika tu kwa kukaa bali kulala usingizi hadi alfajiri ama asubuhi.
Hiyo imekuwa ni mazoea katika maisha ya binadamu na inachukuliwa tu ni jambo la kawaida lakini ukweli ndani yake kuna siri kubwa.
Mtu aweza kujiuliza, je, usingizi ni nini na faida yake ni ipi Ukisoma historia utaona kuwa kwa kipindi kirefu hadi miaka ya 1950, watu walidhani kuwa usingizi ni hali ya kutokuwa na hisia.
Walikuwa na fikra pia katika usingizi uhai unakuwa haupo na katika mwili kila kitu husimama na hakuna



 harakati yoyote inayoendelea. Hata hivyo, wanasayansi mbalimbali wamefanya tafiti nyingi na kubaini kuwa usingizi unapitia hatua mbalimbali.
Moja ya hatua hizo ni akili kuwa katika hali ya kufanya kazi wakati mwili umepoteza hisia kwa kuwa fofofo kwa usingizi.
Kulingana na tafiti hizo, tunapokuwa usingizini, ziko hatua tano tunazopitia. Inasemekana kuwa tunatumia asilimia 50 ya muda wa usingizi katika hatua ya pili, asilimia 20 kwa hatua ya mwisho na asilimia 30 katika hatua ya kwanza, ya tatu na ya nne. Kwa mtoto mchanga hutumia asilimia 50 ya muda wa kulala katika hatua ya mwisho.
Katika hatua hizi tano, hatua ya kwanza kunakuwa na hali nyepesi ya usingizi na kuamshwa kunachukua muda mfupi.
Kwa hatua ya pili kuna kupepesa macho na ubongo hufanya kazi polepole. Hatua ya tatu na ya nne ubongo hupoza kidogo na ni vigumu kumwamsha mtu kwani anakuwa na usingizi mzito.
Wakati huu macho hayajigusi na mtu akiamshwa huchukua muda mrefu kuwa katika hali yake ya kawaida.
Katika hatua ya tano, hali ya kupumua na mapigo ya moyo huongezeka, shinikizo la damu huongezekana.
Muda wa kulala hutegemea mtu na mtu kutokana na mambo mengi hasa umri. Watoto wachanga hulala kwa muda wa saa 16 kwa siku, vijana saa tisa na watu wazima kati ya saa sita na saba, ijapokuwa wengine hulala saa tano kwa siku.
Wanawake wajawazito kuanzia miezi mitatu ya mwanzo wanahitaji muda mrefu wa kulala
- Mwananchi

No comments:

Post a Comment