Kiungo wa Cameroon na West Ham Alex Song amestaafu kucheza
soka la kimataifa baada ya kutotajwa katika kikosi cha timu ya taifa
kitakachocheza Kombe la Mataifa ya Afrika. Kiungo huyo, 27, anayecheza kwa
mkopo kutoka Barcelona sasa ataweza kuendelea kuichezea West Ham baada ya
mazungumzo ya dakika za mwisho na Cameroon kuvunjika. Kupitia Instagram amesema:
"Mapenzi yangu kwa nchi yangu hayatobadilika. Nataka
kuchukua muda na
kuelekeza nguvu zangu kujenga tena fani yangu West Ham United". Song
hajaichezea timu yake ya taifa tangu alipopewa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi
ya Croatia katika ngazi ya makundi katika Kombe la Dunia 2014. West Ham
walikuwa na wasiwasi wa kumkosa mchezaji huyo baada ya kwenda Cameroon kujadili
uwezekano wa kujumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa, kwa ajili ya michuano
ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoanza Januari 17 nchini Equatorial Guinea.
No comments:
Post a Comment