Mkazi mmoja aishiye katika Kitongoji cha Buyumba,Kijiji cha
Bushemba,Kata ya Buganguzi Wilayani Muleba Mkoa wa Kagera anayefahamika kwa
majina ya Godfrey Joseph Kajuna (45miaka) amejinyonga hadi kufa (Kama picha
zinavyoonesha.
Sababu iliyopelekea kifo cha Baba huyo ni baada ya huyo Baba
kumpiga mtoto wake wa kumzaa. Inasemekana kuwa alimpiga na kumjeruhi kichwani
kwa fimbo nzito kisha akamtoboa macho, mtoto huyo anafahamika kwa jina la
Agripina Godfrey (12) anayesoma Darasa la Kwanza ktk S/M Ilambika.
Sasa kisa kizima ni kwamba Baba alitoka ndani na kuwambia
wanae kuwa Mama yao akirudi wasimfungulie mlango…
Hivyo mama aliporudi watoto kwa kumuogopa Baba yao wakakataa
kata kata kumfungulia Mlango.
Basi Mama akaondoka kujiweka sehemu.
Baba yao aliporudi akawauliza Mama yao yuko wapi,ndipo huyo
mtoto aliyeonekana kama ndo mkubwa kwenye familia hiyo akamjibu Baba yake kuwa
"Baba si ulisema mama akija tusimfungulie?" Hali hiyo ikamfanya Baba
yake aanze kumpiga saana! Mpaka kumuumiza vile.
Sasa damu zikaanza kumtoka mtoto,Baba mtoto akachukua Chumvi
na kuanza kuimimina kwenye jeraha kichwani(hiyo nyeupe kwenye Picha)
Basi mtoto alipoonekana kama hali inakuwa Mbaya… Baba
akaandika kijibarua haraka na kusema kuwa kwa kitendo alichofanya na vitendo
vingine ambavyo huwa anaifanyia familia hiyo ameogopa kukamatwa… akajitundika
kwenye Kamba na kujimaliza yeye mwenyewe. Mtoto alipelekwa katika Hospitali
teule ya Wilaya ya Muleba (Rubya Hospital) kwa matibabu zaidi.
Maelezo haya na Picha nimepewa na Afisa Mtendaji Kata ya
Buganguzi Bwana Wilson Dickson.
Credit; Sweetbert Rwabukambara
No comments:
Post a Comment