Wanajeshi wa serikali waliokuwa wakipiga doria katika mji wa
Baga kabla ya Boko haram kuuteka pamoja na kambi ya kijeshi
Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa kundi la Boko Haram
limeuteka mji na kambi moja ya kijeshi inayotumiwa na wanajeshi wa kimataifa
wanaojaribu kukabiliana na wapiganaji hao.
Seneta wa Borno Kazkazini Maina Ma'aji Lawan,eneo la mji wa
Baga amesema kuwa wanajeshi waliitoroka kambi yao baada ya kushambuliwa na Boko
Haram jumamosi asubuhi.
Wakaazi wa Baga,ambao walitoroka kupitia maboti hadi taifa
jirani la Chad,amesema kuwa raia wengi wameuawa na mji huo kuchomwa.
Wapiganaji wa Boko Haram tayari wanadhibiti eneo kubwa karibu
na mji wa Baga,ambao hadi kufikia jumamosi ni miongoni mwa miji michache
iliokuwa imesalia na serikali.
No comments:
Post a Comment