Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, January 13, 2015

Chadema wamtaka Magufuli asiwabague wananchi Chato


Dk. John Magufuli
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Mbunge wa Chato (CCM), Dk. John Magufuli (pichani), kuacha kuwabagua wananchi wa jimbo hilo kutokana na kuwachagua wenyeweviti na wajumbe wa Chadema kupitia Ukawa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14, mwaka jana.
Chadema walitoa tahadhari hiyo baada ya Dk. Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, hivi karibuni kudai atapeleka fedha za Mfuko wa Jimbo katika vijiji na vitongoji walivyoshinda wagombea wa CCM pekee.
Katibu Mwenezi wa Chadema wilayani hapa, Alex Mukama, alisema kutokana na kauli hiyo ya Dk. Magufuli, inaonyesha wazi jinsi asivyofaa kuendelea kuaminiwa na wananchi kwa kuwa anapingana kwa makusudi na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa 



Tanzania inayomtaka kiongozi kujiepusha na ubaguzi wa rangi, itikadi za kisiasa, kidini na kijinsia.
Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Crispin Kagoma, aliwashukuru wananchi hao kwa kudhihirisha wameichoka CCM.
Katika hatua nyingine, Chadema imewaonya wenyeviti wa vijiji na vitongoji kupitia chama hicho kutokubaliana na maamuzi ya serikali ya kuwasumbua wananchi kwa michango ambayo haijapitia kwenye mikutano mikuu ya vijiji na kudhaminiwa na wananchi wenyewe.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mkuyuni, Anacret Lwegoshora (Chadema), alisema baadhi ya viongozi wa serikali kwa kushirikiana na viongozi wa CCM, wamekuwa wakiwashinikiza wananchi kuchangia michango pasipo kuwashirikisha.  

No comments:

Post a Comment