Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, January 16, 2015

Je Irina na Ronaldo wametengana?

 Kuna fununu kuwa Cristiano Ronaldo ametengana rasmi na mlimbwende muonesha vivazi Irina Shayk aliyekuwa mpenzi wake, hili lina pata ithibati baada ya kuonekana Irina ameacha kumfuata Ronaldo katika ukurasa wa Twitter.
Fununu za kuachana kwao zilianza kuzagaa mapema wiki hii kwamba wawili hao wametengana kwa kisa cha Irina kushindwakuonekana kwenye tukio la kupokea tuzo za Ballon d'Or usiku wa jumatatu ambapo Ronaldo alikuwa mshindi wa jumla.
Irina amezoeleka kuonekana mstari wa mbele kila wakati na kikosi cha Real Madrid katika matukio yote na taarifa za hivi karibuni kwenye chombo cha habari cha Ki Hispania kinaeleza sababu za Irina 


kutoonekana katika tuzo hizo kuwa ni kutokana na mahusiano yao kufukia tamati .
Gazeti la masuala ya michezo la El Mundo Deportivo linaeleza kwamba suala la kuachana kwao ni kama limethibitishwa kutokana na Irina kuto mfuata Ronaldo kwenye mtandao wa Twitter kama ilivyozoeleka.

No comments:

Post a Comment