Mheshimiwa Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini
mwanzoni mwa mwaka 2014 alikua na mgogoro mkubwa na Chama chake cha
Chadema.Magazeti yaliyotoka siku chache zilizopita yali ripoti taarifa ya
Mbunge Zitto Kabwe kurudi tena Chadema,hiki ndicho alichokisema Zitto Kabwe.
Swali lilikua ni yeye kuhusu kurudi Chadema>>’Hapana
nadhani hizo ni tetesi kwa sababu sijatoa kauli yoyote kuhusiana na hilo na
moja mimi bado mwanachama wa Chadema kwa sababu nina kesi mahakamani na kesi
hiyo
haijaamuliwa,bado inaendelea’
‘Sijawahi kutoka kwenye uanachama wa Chadema,mtu anaposema
nataka kurudi Chadema hayuko sahihi,inafahamika nilikuwa na matatizo na chama
hatujaweza kuyatatua,hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanyika lakini kuna
baadhi ya watu wameanza kuleta hayo mazungumzo’.
No comments:
Post a Comment