Wafanyabiashara wanaondesha shughuli zao za kibiashara katika masoko zaidi ya matano yaliyopo Jijini Mbeya wakiwa kwenye maandamano kuelekea mahakamani wakishinikiza mahakama hiyo kumuachia huru, Mwenyekiti wa Soko la Soweto Honola Mbogella ambaye alifikishwa mahakamani hapo na halmashauri ya jiji la Mbeya kwa tuhuma za kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao.
Wafanyabiashara wanaondesha shughuli zao za kibiashara katika masoko zaidi ya matano yaliyopo Jijini Mbeya, wakiwa nje ya mahakama ya Mwanzo ya Mbeya mjini wakishinikiza Mwenyekiti wa Soko la Soweto kuachiwa huru.
Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa
MWENYEKITI wa Soko la Soweto jijini Mbeya, Honola
Mbogella amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo Mbeya mjini kwa tuhuma za
kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao.
Kufuatia kukamatwa
kwa Mwenyekiti huyo kulisababisha zaidi ya wafanyabiashara 1000 wanaondesha
shughuli zao za kibiashara katika masoko matano yaliyopo Jijini Mbeya,
kuandamana na kuizunguka mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini, wakishinikiza
mahakama hiyo kumuachia huru.
Mwenyekiti huyo amefikishwa katika
mahakama ya Mwanzo ya Mbeya mjini leo na kesi yake kusikilizwa majira ya saa
tatu asubuhi ambapo kesi hiyo ilivuta hisia za watu kutokana na kundi hilo
la wafanyabiashara kuizunguka mahakama hiyo, huku jeshi la polisi likilazimika
kuimarisha ulinzi.
Akisomewa mashitaka hayo Mbele ya Hakimu wa Mahakama
ya mwanzo ya Mbeya Mjini Ubaswege Mathew, karani wa Mahakama hiyo, Sioni
Kasunga alisema mtuhumiwa huyo alifanya kosa hilo January 10 mwaka huu akiwa
katika eneo lake la kazi la soko la
Soweto lililopo Jijini Mbeya. Alisema kwa mujibu wa kifungu kidogo cha sheria namba 101(a) sura ya 288 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mtuhumiwa aliwazuia watumishi wa umma wa halmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya kazi yao ya kukusanya ushuru.
Soweto lililopo Jijini Mbeya. Alisema kwa mujibu wa kifungu kidogo cha sheria namba 101(a) sura ya 288 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mtuhumiwa aliwazuia watumishi wa umma wa halmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya kazi yao ya kukusanya ushuru.
Alisema, mtuhumiwa aliwazuia wafanyabiashara
hao kugoma kutozwaushuru wa shilingi 200 hadi 300 na halmashauri ya Jiji
la Mbeya kwa maelezo kwamba licha ya wafanyabiashara hao kulipia tozo hiyo
kwa kipindi kirefu bado soko hilo limeendelea kukithiri kwa uchafu.
Aidha,
kutokana na kosa hilo, Hakimu wa mahakama hiyo, Ubaswege Mathew baada ya
kusikiliza maelezo hayo alitoa nafasi kwa mtuhumiwa ambaye alikana shitaka hilo
hivyo, hakimu kuhairisha kesi hiyo mpaka kesho na na kusema kuwa dhamana kwa mtuhumiwa ipo wazi.
“Kesi hii nimeihairisha mpaka kesho asubuhi, mtuhumiwa anahaki ya kuwekewa dhamana kwa masharti ya kiasi cha fedha
cha shilingi milioni mbili na wadhamini wawili mmoja akiwa ni mtumishi wa serikali,”alisema Wakati kesi hiyo ikiendelea mahakamani hapo, umati mkubwa
wa wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao katika masoko matano ya
Soweto,Uyole, Mabatini, Sokomatola na Uhindini ulijitokeza na kuizunguka
mahakama hiyo kwa kile walichokidai kwamba wenyekityi huyo
ameonewa.
Wakizungumza na Mbeya yetu nje ya mahakama, wafanyabiashara hao
ambao waligoma kutaja majina yao, walisema wao wamegoma kulipa ushuru huo
kutokana na halmashauri kushindwa kuetekeleza majukumu yao ya ukarabati wa
miundombinu pamoja na usafi wa mazingira hivyo Mwenyekiti huyo hausiki na
suala la kuwashawishi kugoma kama inavyodaiwa na halmashauri.
Hata
hivyo, wafanyabiashara hao wamegoma kuendelea na shughuli zao mpaka suala hilo
litakapo patiwa ufumbuzi kwa halmashauri kurekebisha miundombinu na usafi wa
mazingira katika maeneo yabiashara.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment