Nchi ya Ubelgiji ilipitisha sheria ya watu wanaotaka kufa
kusaidiwa kwa kudungwa sindano kwa miaka 12 iliyopita.
Frank Van den Bleeken aliwasilisha ombi lake kwa Serikali ya
nchi hiyo kwamba asaidiwe kufa kwa kudungwa sindano yenye sumu ili kumwepushia
msongo wa mawazo anaokabiliwa nao kutokana na kukabiliwa na kesi ya mauaji na
ubakaji.
Wizara ya Sheria Ubelgiji kupitia kwa Waziri wake Koen Geens
amesema anaheshimu ushauri wa madaktari wanaomtibu mtuhumiwa huyo aliyeiomba
Serikali kumsaidia kifo chake.
No comments:
Post a Comment