Makamanda wa polisi wa mikoa mitatu ya simiyu, shinyanga na mwanza
wamefanikiwa kuvunja mtandao hatari wa ujambazi uliokuwa unaongozwa na
mfanyabiashara wa mjini bariadi Njile Samwel huku makachero wa jeshi
hilo katika mikoa ya kanda ya ziwa pia wakikamata watuhumiwa watano,
bunduki moja ya SMG, risasi 331 na mifupa inayodaiwa kuwa ya binadamu.
Kamanda wa polisi mkoani mwanza, SACP Valentino Mlowola, akiwa
ameambatana na kamanda Justus Kamugisha wa mkoa wa shinyanga pamoja na
Charles Mkumbo wa mkoa wa simiyu wanajitokeza kwa waandishi wa habari
kuelezea tukio la
kukamatwa kwa njile samwel ambaye amekuwa na tabia ya kunzisha mtandao wa uhalifu na kisha kuwaua kama mbinu ya kukwepa wapelelezi.
kukamatwa kwa njile samwel ambaye amekuwa na tabia ya kunzisha mtandao wa uhalifu na kisha kuwaua kama mbinu ya kukwepa wapelelezi.
Kamanda wa polisi mkoa wa simiyu Charles Mkumbo anaeleza namna
ambavyo kiongozi huyo mkuu wa mitandao ya ujambazi kanda ya ziwa
alivyoweza kumuua mshirika mwenzake wa ujambazi chambalu nkono kwa
kutumia silaha aina ya smg iliyokuwa na magazini yenye risasi 40 ndani
ya pori la akiba la maswa.
Kuhusu tukio la kutekwa kwa mtoto pendo emanuel mwenye ulemavu wa
ngozi wa ngozi lililotokea desemba 27 mwaka jana katika kijiji cha ndami
wilayani kwimba., kamanda wa polisi mkoani mwanza valentino mlowola
amesema polisi inaendelea kuwashikilia watuhumiwa wanane akiwemo baba
mzazi wa mtoto huyo baada ya mchujo kufanyika huku akisema jeshi hilo
halitashindwa kumpata mtoto huyo akiwa hai au hata amekufa.
No comments:
Post a Comment