mavumba yaliyokuwemo hayakuguswa
Dubai imejinyakulia sifa ya kipekee katika kupima Imani za
jamii kwa pochi iliyoangushwa mtaani,na mara ikarejeshwa kwa mhusika mara moja.
Katika utafiti uliofanywa na mtengeneza Filamu mwenye asili
ya Uingereza katika mitaa ya Dubai, alijaribu mara arobaini na tano kuidondosha
kwa makusudi na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi hiyo
kwa mmiliki wake.
Daniel Jarvis, mwenye miaka 26,akiwa ameificha kamera yake
na kurekodi mfululizo wa matukio hayo ya makusudi akiwa pamoja na rafikiye
aliyejipachika
jina la utani la 'Digi' ama Dan, mwenye miaka 25, walibarizi
katika viunga vya Downtown na Bur vilivyoko Dubai,siku za karibuni na kuweka
swali je unaweza kuiba Dubai? Kutaka kuichunguza jamii na kurushwa vipande
vyake katika YouTube ambapo mpaka kufikia jana usiku watazamaji walikuwa ni
zaidi ya 70,000 .
Jarvis aliiambia 7DAYS walishangazwa na utafiti huo na
kikubwa kilichowasangaza ni kwamba waliookota pochi hiyo hawakujishughulisha
kutazama ndani kuna nini? Wakati pochi hiyo ilikuwa imesheni euro za kutosha na
fedha ya Falme za Kiarab dirham kadhaa.
Mtaa wa kwanza walioufanyia majaribio ni mtaa uliko katika
barabra ya Sheikh Zayed karibu na soko kuu la kibiashara na jirani kabisa na
mnara wa Emirates lakini kila aliyeiona pochi hiyo aliirejesha,lakini baadaye
tukafikiri sababu ya kurejeshwa pochi hiyo kuwa walioko eneo hilo ni matajiri.
Basi utafiti wetu tukauhamishia eneo la Bur ,Dubai, mahali
ambapo palionekana duni kidogo cha ajabu watu waliendeleza utamaduni ule ule wa
kurejesha pochi kama ilivyo, na hali eliendelea hivyo mara kadhaa.
Jarvis anasema wameshafanya utafiti kama huo katika mji wa
London nchini Uingereza. Na huko walistaajabu walipoidondosha tu aliyeiokota
alianza kukimbia nayo wa nako hakuna aliyethubutu kuichukua pochi hiyo.
Jarvis, alivalia suti nadhifu na kuigiza kudondosha pochi
anaonekana kwenye video hiyo anaeleza hisia za kurejeshewa kitu ulichondondosha
kuwa ni raha iliyoje .lakini akaendelea kusema kuwa anadhani vyombo vya habari
hupotosha ukweli,kwakuwa kulikuwa na kichwa cha habari kuwa kuna mtu
alihukumiwa miaka 15 jela kwa kuiba mdoli wenye taswira ya dubu, utafiti wetu
umegundua tofauti na wayasemayo.
Trollstation ina wanachama wapatao 230,000 na utafiti wao
kutoka Falme za Kiarab unaelekezwa Ulaya, Marekani na hatimaye Afrika .
Inawezekana katika maeneo watakayopita kuvunja rekodi ya
Dubai tusubiri wakati uwadie, ni kauli yake Jarvis .
No comments:
Post a Comment