Mgogoro
kati ya Wakulima na Wafugaji katika bonde la Mgongola , wilayani
Mvomero mkoani Morogoro umeibuka tena na kusababisha kifo cha mkulima
mmoja na wengine 14 kujeruhiwa.
Waliojeruhiwa wamekatwa sehemu mbalimbli za miili yao na mapanga na sime za wafugaji.
Kati
ya wakulima waliojeruhiwa kwenye tukio hilo lilitokea jioni ya Januari
16, mwaka huu ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani,
Ally Ambilikila na familia yake .
Hata
hivyo baada ya kumvamia walimpora fedha taslim Sh milioni tatu na
kumchomea moto nyumba iliyokuwa ndani ya eneo la shamba lake.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonald Paulo, alithibitisha kutokea kwa
mapigano hayo na kumtaja aliyeuawa kuwa Abdallah Shomari (27) mkazi wa
Msamvu Manispaa ya Morogoro ambaye alikuwa ndani ya shamba hilo na
kupigwa kwa marungu na wafugaji hao.
Kamanda
Leonald amesema katika tukio hilo tayari jeshi la Polisi limefanikiwa
kuwakamata wafugaji wawili wa Kimasai ambao ni Kisaingwa Mbingwa na
Rashid Saliku wote wakazi wa kijiji cha Kambala wilayani Mvomero.
Alisema
kwamba siku ya tukio wakulima waliamua kwenda kuandaa mashamba na
baadaye wafugaji walienda katika eneo hilo na kutokea mzozo mkubwa
kipindi cha mchana ambapo jioni yake kukatokea mapigano hayo.
Kwa
upande wa Kamanda mstaafu Ambalikila akielezea tukio hilo la kuvamiwa
na wafugaji , alisema kuwa siku hiyo walienda katika bonde hilo ambalo
wanalima tangu miaka 60 iliyopita kwa ajili ya kuanza kutayarisha
mashamba ya mpunga kwa msimu huu.
Alisema
kuwa wakati wakiendelea kulima kwa kutumia trekta la kukodi ghafla
lilitokea kundi kubwa la jamii ya wafugaji wa Kimasai wa kijiji cha
Kambala na kuvamia eneo hilo.
Alisema
mara baada ya kuwavamia wafugaji hao waliwapiga kwa kutumia sime, fimbo
na mapanga sehemu mbalimbali akiwemo yeye pamoja na familia ya watu
kumi waliokuwa shambani kwa ajili ya matayarisho ya shamba.
Kamanda
huyo mstaafu wakati wafugaji hao wakiendelea kuwapiga baadhi yao
walimpora fedha taslimu Sh milioni 3, simu na kuchoma magunia 20 ya
mbegu ya mpunga iliyokuwa tayari kwa kupandwa katika shamba lake.
Hata
hivyo alisema baada ya tukio hilo wafugaji hao waliondoka na wao kupata
msaada kutoka kwa wananchi na kuwafikisha kituo cha Polisi na baadaye
kufikishwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu.
Naye
Said Ambilikila ambaye ni mtoto wa Kamanda huyo mstaafu aliyelazwa
katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, alisema kuwa alipigwa
kichwani na mkononi na wafugaji hao kwa kutumia silaha hizo za jadi
baada ya kuvamiwa wakiwa katika shamba lao.
Kwa
upande wa Costa Augustino mkazi wa kijiji cha Dihombo wilayani Mvomero
ambaye naye amelazwa akipatiwa matibabu kutokana na kukatwa mapanga
katika mikono yake yote miwili na sehemu ya kichwani alisema baada ya
kupambana na wafugaji hao alilazimika kutumia mbinu za kujifanya kuwa
amekufa na wafugaji hao kuondoka.
Alisema
kuwa baada ya wafugaji hao kuona kuwa amekufa walitawanyika na yeye
alijivuta mpaka katika kibanda na baadaye kuja kuokolewa na askari wa
jeshi la Polisi waliofika eneo hilo baada ya kupata taarifa.
Baadhi
ya majeruhi wengine waliolazwa katika hospitali hiyo ni Rajabu Ally,
Mohamed Ramadhan na Ramadhani Salum wote wakazi wa kata ya Kinguruwila
manispaa ya Morogoro.
Wakizungumza
wadini hapo Mohamed Ramadhan alisema baada ya kupigwa aliporwa na
wafugaji kiasi cha Sh 150,000 pamoja na simu ya mkononi, wakati
Ramadhani Salum alidai kuporwa kiasi cha Sh 850,000 na kuchomewa
pikipiki pamoja na nyumba yake iliyokuwa shambani kwake.
Msimamizi
Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro,Elias Kilela,
alithibitisha kupokea majeruhi saba waliohamishiwa katika hospitali hiyo
baada ya kujeruhiwa na Wafugaji katika Bonde la Mgongola.
Alisema
kuwa majeruhi hao wamelazwa wadi namba moja hospitalini hapo huku
wakiwa wamekatwakatwa na mapanga katika maeneo yao mbalimbali ya mwili
na wanaendelea vizuri baada ya kuanza kupatiwa matibabu huku mmoja
ambaye ni Kamanda mstaafu wa Polisi akiruhusiwa.
Awali
Mwenyekiti wa kijiji cha Mkindo Patrick Longomeza ambaye ni miongoni
mwa wakulima wanaolima katika bonde hilo la Mgongola alithibitisha
baadhi ya wakulima kutoka katika kijiji chake kujeruhiwa na wafugaji
baada kuvamiwa wakiwa katika bonde hilo.
Alisema wakulima hao walienda katika bonde hilo kwa ajili ya kuandaa mashamba ya mpunga ambalo wamekuwa wakilima kwa muda mrefu.
Alisema
kuwa baada ya kupata taarifa walienda katika eneo la tukio na
kuwakimbiza katika hospitali za Bwagara na wengine kituo cha afya cha
Mvomero huku baadhi wakiwakimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Morogoro ambako baadhi yao wamelazwa kwa ajili ya matibabu.
No comments:
Post a Comment