Watu watano akiwamo mtoto wa miaka 15, wamejeruhiwa
baada ya kushambuliwa kwa bomu la mkono lililotupwa kwenye banda la
kuonyeshea picha za video.
Bomu hilo linadaiwa kuwa ni la kutengenezwa kienyeji, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Frasser Kashai.
Pamoja na shambulio hilo, watu wengine watatu wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa katika matukio tofauti ya ajali na kuuawa.
Kamanda wa Polisi Mkoa akizungumzia bomu alisema ni la kurushwa kwa mkono na kwamba lilivurumishwa alhamisi saa 2 usiku, kwenye kibanda cha kutizamia picha za video kilichoko kijiji cha Amboni na kujeruhi watizamaji watano.
Waliojeruhiwa ni Hassan Abdallah (72), Rashid Ally (45), Mrisho Abdi (29) mtoto Juma Mtoo (15) na Abdul Ismael (19) wote wakazi wa kijiji cha Amboni.
Kashai alisema wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga, Bombo wakiwa na majeraha mbalimbali mwilini na kwamba Ally Rashid (25) mkazi wa kijiji hicho anashikiliwa kwa uchunguzi.
Rashid anahusishwa na bomu hilo linalodaiwa ni la kutengeneza kienyeji kwa mujibu wa Kamanda.
Wakizungumzia tukio la bomu hilo, baadhi ya wananchi waliokuwa eneo la tukio walieleza kuwa waliona kitu chenye mwanga angani kabla ya kutua kwenye banda ambalo walikuwemo watu zaidi ya 30 wakifurahia picha za video.
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kutokuwa na hofu ya tukio hilo na kwamba hali ya usalama imedhibitiwa huku uchunguzi wa kina ukiendelea na kuhimiza ushirikiano baina ya wananchi na jeshi hilo kukabiliana na uhalifu.
Katika tukio jingine, mtuhumiwa George Nambai, ameuawa na watu wenye hasira baada ya jaribio lake la kutaka kupora simu kushindwa.
Aliuawa baada ya kushindwa kuiba badala yake wananchi wenye hasira walijitokeza kumshambulia hadi kufa.
Kamanda Kashai alisema aliuawa juzi katika eneo la Central baada ya kumchoma kitu chenye ncha kali ubavuni Mohamed Abraham ili kumnyang’anya simu, hata hivyo mmiliki huyo wa simu naye alifariki wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Bombo.
Kamanda Kashai alisema tukio jingine ajali ya gari lenye aina ya Isuzu iliyokuwa ikiendeshwa na Mngazija Shabani, ilipinduka na kusababisha kifo cha abiria mmoja na kujeruhi wengine wanne.
Ajali hiyo ilitokea Shume wilayani Lushoto na aliyepoteza maisha ni Irene Emanuel (14) na waliojeruhiwa ni Irene Grayson (16), Rose Elieza (30), Eva Mbonea (28) na Emilia Elineema wote wakazi wa Mavumo Shume wilayani Lushoto. Ajali hiyo ilihusisha gari namba T 618 AHT.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment