Mbwa aliyetelekezwa nchini Scotland ajulikanaye kwa jina la
Kai amepatiwa ofa tele za makazi mapya.
Mambo yanaonekana si mabaya kwa mbwa aliyetelekezwa kwenye
stesheni ya Treni akiwa na sanduku lenye mahitaji yake.
Mbwa huyu alikutwa katika Stesheni akiwa amefungiwa kwenye
reli siku ya ijumaa juma lililopita.
Lakini wasamaria waliomnasua katika eneo hilo wanasema
wamekuwa wakipigiwa simu mara nyingi
na watu wakitaka kumpa makazi mbwa huyo.
Wasamaria wema hao wanasema Kai yuko katika hali nzuri na ni
rafiki hivyo wanaamini kuwa wamiliki wa mbwa huyo ambao bado wanatafutwa
walishindwa kumhudumia.
Taasisi hiyo ya msaada wa wanyama inatoa wito kuwasiliana
nao kupitia namba ya msaada 03000 999 999 ikiwa kuna mtu atakuwa na taarifa
kuhusu wamiliki wa Kai.
No comments:
Post a Comment