Ajali ya ndege
Mtoto mmoja wa miaka saba ametembea hadi katika nyumba moja
katika jimbo la Kentucky nchini Marekani ili kuripoti kuanguka kwa ndege
aliyoabiri.
Kulingana na polisi ndege hiyo baadaye ilipatikana imeanguka
huku watu wanne wakiwa wamefariki katika kaunti ya Lyon yapata kilomita 50
mashariki mwa mji wa Paducah
Kituo cha runinga cha NBC nchini Marekani kimesema kuwa
msichana huyo alimwarifu mtu aliyemfungulia mlango kwamba wazazi wake
walifariki katika ajali hiyo ya ndege.
Picha ya ndege hiyo haijatolewa na polisi hawajatoa
tamko
lolote kuhusu uhusiano wake na waathirwa.
Shirika linalosimamia anga za juu limesema kuwa maafisa
wanaodhibiti usafiri wa ndege walipoteza mawasiliano na ndege hiyo aina ya Piper
PA-34 baada ya rubani kuripoti matatizo ya mitambo.
Dakika 30 baada ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano ,mkaazi
mmoja wa Lyon kaunti aliwapigia simu polisi kuwaarifu kuwa msichana huyo
aliwasili katika nyumba yake ili kuripoti kuhusu ajali hiyo.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment