Christiano Ronaldo akisherehekea bao lake dhidi ya Barcelona
Aliyekuwa msaidizi wa kocha wa Manchester united Mike Phelan
anaamini kuwa Cristiano Ronaldo huenda akaandikisha mkataba wa kurudi katika
kilabu ya Old Trafford katika siku sijazo.
Ronaldo amehusishwa na mpango wa kurudi Manchester United
katika muda wake katika kilabu ya Real Madrid ,lakini mpango kama huo haujazaa
matunda kufikia sasa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye
alichezea Man U
anafurahia maisha yake katika kilabu ya Real Madrid lakini Phelan anaamini
huenda akashawishika kurudi katika ligi ya Uingereza.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment