Kwa Triple D, changamoto kubwa kwake ni kununua nguo za
ndani ambazo zinamtosha
Mwanamume mmoja mwenye uume mbili, amezungumza na BBC kuhusu
anavyoiishi na hali yake hio.
Anajulikana tu kama 'Triple D,' na ana umri wa miaka 25
kutoka nchini Mashariki mwa pwani ya Marekani na anadai kuwa amekuwa na
uhusiano wa kimapenzi na wanawake 1,000.
Mwanamume huyu anaugua ugonjwa ujulikanao kama 'Diphallia'
ambapo mwanamume anazaliwa na uume mbili.
Kulingana na shirika la kimataifa la afya,BMJ, mwanamume
mmoja kati ya milioni tano, duniani huzaliwa na hali hio.
ONYO: Taarifa hii ina lugha ambayo kwa baadhio
huenda
ikawachukiza
"maisha yangu hayatawahi kuwa sawa tena ikiwa
nitajitambulisha kwa dunia nzima, '' alisema Triple D.
Hata hivyo BBC ilikubali kubana jina lake na hata
kutoonyesha sura yake.
Anasema hataki kuwa kichekesho kwa jamii hasa anakoishi.
Katika siku za uchanga wake, wazazi wake walimwambia
kutokana na maumbile yake , yeye alikuwa mtoto mwenye maumbile ya kipekee.
Anakumbuka wazazi wake wakimketisha chini na kuanza
kumuelezea kwamba asidhubutu kucheza mchezo wa 'kalongo' na watoto wenzake na
wala asidhubutu kuvua nguo zake za ndani mbele ya watu wengine.
'Mawaidha ya wazazi'
Kutokana na mawaidha ya wazazi wake, aliweza kuweka hali
yake kama siri kubwa sana, lakini alipokuwa katika shule ya upili wanafunzi
wenzake waligundua siri hio na hapo anasema alipitia masaibu si haba.
''Mwanzoni, sikutaka watoto wengine shuleni kujua hali yangu
kwani sikutaka kumuudhi yeyote. ''
Natamani sana wazazi wangu wangeniambia na kunitahadharisha
kuwa watu huchekelea kitu wasichokielewa.
''Sikutaka wanaume wenzangu kuhisi vibaya kwamba hawana uume
mbili kama mimi na kuanza kunionea kijicho, au kuanzia kunifanyia stihizai na
kunichekelea kwamba mimi sio mtu wa kawaida'' alisema 'Triple D'.
Alipokua na umri wa miaka 16, alitaka kufanyiwa upasuaji na
kuondolewa uume mmoja kwa sababu watu hasa wasichana walianz akunitazama sana
katika sehemu yangu ya siri.
''Natamani sana wazazi wangu wangenishauri kuhusu hali yangu
basi nisingeopa gata kidogo.''
Alijohiwa kwa nini ni rahisi kwake kuzungumzia hali yake
wakati akiendelea kubana jina lake? Alijibu na kusema kila mahali ninapokwenda,
kila mtu atanifahamu na kuwa na matarajio makubwa kwangu.
Triple D amechapisha kitabu kwa jina: ''Double Header: My
Life With Two Penises'', yaani maisha yangu na uume mbili pamoja na anavyokabiliana
na hali yake. Anasema sehemu zake hizo zinafanya kazi vyema na kwamba
hajabahatika kuwa na uhusiano wa kimapenzi uliodumu kwa mda mrefu.
Kwake changamoto kubwa ni kununua nguo zake za ndani.
No comments:
Post a Comment