WEKUNDU wa Msimbazi wamefanikiwa kufuzu hatua ya robo
fainali ya kombe la Mapinduzi kufuatia kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
vinara wa ligi ya Zanzibar, JKU katika mechi iliyomalizika usiku huu uwanja wa
Amaan Zanzibar.Bao pekee la Simba limefungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’
katika dakika ya 11 kwa shuti kali
akipokea pasi murua ya Said Ndemla.
Kikosi cha JKU kilichoanza
Kwa matokeo hayo, Simba wameibuka vinara wa kundi C kwa
kujikusanyia pointi 6 kibindoni, huku nafasi ya pili ikishikwa na Mtibwa Sugar
wenye pointi tanoSimba walianza mchezo kwa kasi, lakini JKU walionekana
kuchakarika kuwadhibiti wakali hao wa Msimbazi.Kikosi cha Mnyama kinachonolewa
na
Mserbia Goran Kopunovic kimeonekana kucheza mpira wa kasi na pasi za uhakika
kuanzia sehemu ya ulinzi na safu ya ulinzi.Baada ya mechi hiyo, kocha Kopunovic
amesema timu yake inaimarika kidogo kidogo na ilicheza tofauti kwa vipindi
vyote.
“Hii ni siku ya tano tu tangu nifike, bado naendelea kuwapa
mbinu mpya. Wachezaji wangu kimbinu nawaona wazuri”
“Mimi napenda vijana ndio maana nawatumia wengi. Kidogo
kidogo tutakuwa safi” Alisema Kopunovic.
Simba wanasubiri mpinzani wao wa Robo fainali katika mechi
za kesho ambapo kutakuwa na mechi nne.
Majira ya saa 9:00 alasiri katika uwanja wa Amaan, KCC
watachuana na KMKM, saa 11:00 jioni Azam fc watakabiliana na Mtende, hizo ni
mechi za kundi B.
Kundi A, Taifa ya Jang’ombe itapepetana na Polisi katika
uwanja wa Mao Dze Tung majira ya saa 9:00 alasiri.
Mtanange mwingine wa kundi A utawakutanisha Yanga dhidi ya Shaba
majira ya saa 2:00 usiku uwanja wa Amaan.NA SHAFFIH DAUDA
No comments:
Post a Comment