Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, January 20, 2015

TAZAMA PICHA 5ZA WANAFUNZZI WALIPONDAMANA KUPINGA UVAMIZI KWENYE KIWANJA CHAO,POLISI WAJERUHIWA

 Polisi nchinikenya katiika mji mkuu Nairobi leo imewafyetulia gesi ya kutoa machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchezea na mmiliki binafsi.
Polisi hao wakiwa na Mbwa waliwatawanyta wanafunzi hao, baadhi yao wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka sita baada ya kuuangusha ukuta mpya uliojengwa kati ya shule yao na uwanja huo.
 Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma walipopata kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na hata kuwekwa uzio.
Shule hio ina karibu watoto 1,000 walo kati ya umri wa miaka mitatu na kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji.
 Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma
Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa katika purukushani hilo wakati polisi walipoingilia kati na kujaribu kuwatawanya wanafunzi hao waliokuwa wanazua rabsha.
Baadhi yao walipelekewa hospitalini baada ya kupata majeraha madogomadogo.
Baadhi ya wanafunzi hao walikabiliana na polisi wakiwa wamebeba vijiti na kuwanyoshea.
 Polisi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa kwa mawe.
Walimu wa shule hio pia waliandamana wakisaidiwa na wanaharakati wa kisiasa.
Haijajulikana ambavyo mtu huyo aliweka uzio katika kiwanja hicho walichokuwa wakitumia wanafunzi kuchezea


 Wanafunzi wakigonga uzio uliokuwa umewekwa katika ardhi hio iliyonyakuliwa na mtu asiyejulikana
Baraza la jiji limesema kuwa ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa halijazungumzia ambavyo ardhi yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati wanasema kiwanja hicho kimeuzwa kwa tajiri anayepanga kukitumia kwa ujenzi.

No comments:

Post a Comment