Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, January 8, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA - DIRISHA DOGO LA USAJILI

Chelsea wanajiandaa kulipa pauni milioni 200 kutengua kipengele cha mkataba ili kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 27, (Daily Star), Liverpool wanataka kumnunua kiungo wa Manchester City James Milner, 29, ambaye mkataba wake unakwisha mwisho wa msimu (Times), Manchester United wametangaza dau kutaka kumsajili beki wa kati wa Ujerumani Mats Hummels, lakini Borussia Dortmund wanasema mchezaji wao huyo, 26, hauzwi (Daily Express), wakati huohuo Man Utd itaendeleza mazungumzo na kipa David De Gea,24, baada ya kusajiliwa kwa Victor Valdes kwa mkataba wa miezi 18 (Daily Mail), kipa wa Chelsea Petr Cech, 32, huenda akaondoka Darajani mwisho wa msimu na amehusishwa na kuhamia Arsenal 


(Telegraph), winga wa England Andros Townsend, 23, amesisitiza kuwa atabakia Tottenham, licha ya kuhusishwa na taarifa za kuondoka White Hart Lane (London Evening Standard), dau la Arsenal la pauni milioni 5 kumsajili kiungo Marcelo Brozovic, 22, limekataliwa na Dinamo Zagreb. Everton, Liverpool, Tottenham, AC Milan na Valencia pia zinamnyatia mchezaji huyo (Daily Star), meneja mpya wa Crystal Palace, Alan Pardew, anataka Rickie Lambert wa Liverpool kuwa moja ya usajili wake wa kwanza (Guardian), Aston Villa wameanza mazungumzo na Manchester City kuhusiana na kumsajili winga Scott Sinclair, 25 (Sky Sports), Olympiakos ya Ugiriki imejaribu kumsajili mshambuliaji wa Italy na Liverpool Mario Balotelli,24, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu (Daily Express), kiungo wa Liverpool, Suso, 21, anajiandaa kujiunga na AC Milan kwa mkataba wa miaka minne (Talksport), Tottenham wapo tayari kumwachilia Emmanuel Adebayor, 30, kwenda ligi ya MLS ya Marekani, ili kupanga upya safu ya ushambuliaji (Times), Manchester United huenda wakamkosa kiungo anayetajwa kuwa na kipaji kikubwa Martin Odegaard, 16, kutoka Norway, ambaye huenda akahamia Real Madrid (Manchester Evening News). Katika habari nyingine-

Alan Pardew huenda aliondoka Newcastle kwa sababu aliambiwa na mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley kuwa anataka kuiuza timu (Telegraph), Steven Gerrard wa Liverpool anadhani Jordan Henderson, 24, atakuwa chaguo bora kuwa nahodha mpya (Sun), Ligi Kuu ya England itaanza mapema kwa wiki moja msimu ujao ili kuhakikisha mechi chache zinachezwa kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya (Daily Star)- na hatimaye Chelsea walikosa nafasi ya kumsajili Edin Hazard kwa pauni laki moja wakati akiwa na umri wa miaka 16. Kiungo huyo kutoka Ubelgiji ambaye sasa ana miaka 24, alijiunga na Chelsea kwa pauni milioni 32 mwaka 2012. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Habari za usajili zilizothibitishwa nitakujulisha pindi zitakapothibitishwa.

No comments:

Post a Comment