Kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdes amekubali kujiunga
na Manchester United. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Spain, ambaye amekuwa
akifanya mazoezi na Manchester United katika jitihada za kupona jeraha la goti,
amekubali mkataba wa miezi 18. Valdes, 32, alishinda makombe sita ya La Liga,
na matatu ya Champions League akiwa na Barcelona, kabla ya mwisho wa msimu
uliopita ambapo mkataba wake ulimalizika. Mkataba huu huenda ukasababisha kipa
wa akiba wa United
Anders Lindegaard kuondoka Old Trafford. Hatua hiyo pia
inaleta maswali mengi kuhusu hatma ya David De Gea, 24, ambaye alikuwa mchezaji
bora wa timu hiyo msimu uliopita na amekuwa aking'ara msimu huu pia.
Mkataba wake utaisha mwaka 2016, ingawa taarifa kutoka
United zinasema hawana wasiwasi na kipa huyo kuongeza mkataba wake.
No comments:
Post a Comment