TAARIFA KWA UMMA
Kuna uvumi unazagaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii kuwa mmiliki wa VIP Enginering and Marketing Limited, “aliyekuwa anamiliki hisa IPTL Ndugu Rugemalira” amefungua kesi Mahakama Kuu akiidai Serikali jumla ya TShs. 398 bilioni.
VIP Engineering and Marketing Limited inapenda kuufahamisha umma kuwa hizi taarifa si za kweli, hakuna kesi yoyote ambayo imefunguliwa na VIP Engineering and Marketing Limited au Bw. James Rugemalira dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mahakama Kuu ya Tanzania au Mahakama nyingine yoyote.
VIP Engineering and Marketing Limited inaamini uvumi huu unalenga kuleta uchonganishi wa VIP Engineering and Marketing Limited kwa umma ili kukidhi maslahi binafsi ya waanzilishi wa uvumi huo.
VIP ENGINEERING AND MARKETING LIMITED
03 JANUARI, 2015
No comments:
Post a Comment