Diafra Sakho wa West Ham na Senegal
Mchezaji Diafra Sakho na kilabu ya West Ham zinakabiliwa na
uchunguzi kutoka shirikisho la soka duniani FIFA kufuatia hatua ya mchezaji
huyo kujiondoa katika kikosi cha Senegal katika michuano ya kombe la mataifa ya
Afrika.
FIFA inasema kuwa imefungua uchunguzi wa kinidhamu kwa
kukiukwa kwa sheria.
Sakho 25,alijiondoa akiwa na jeraha la mgongo ,lakini
baadaye akaifungia bao West Ham katika mechi yake ya FA dhidi ya Bristol City.
Sheria za FIFA zinasema kuwa mchezaji hawezi kuichezea
kilabu yake iwapo anatakikana kuichezea timu yake ya taifa,lakini West Ham
imekana kufanya makosa yoyote.
No comments:
Post a Comment