Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, February 26, 2015

JAJI MKUU AWASILI MKOANI TABORA KATIKA ZIARA YA KIKAZI


Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akisalimiana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Simba alipowasili MKOANI Tabora kwa ajili ya ziara ya kutembelea Mahakama mkoani humo.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akisalimiana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Bi. Suzan Kaganda alipowasili mapema mkoani Tabora kwa ajili ya ziara.


Baadhi ya Watumishi wa Mahakama mkoani Tabora wakisubiri kumpokea Mhe. Jaji Mkuu .
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akipata Maelezo mafupi kutoka kwa Mhe. Amir Mruma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu (aliyesimama) Kanda ya Tabora alipowasili katika jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kuanza rasmi ziara yake ya kikazi. Wengine walioketi ni Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora. (Picha na Mary Gwera, Mahakama).

No comments:

Post a Comment