Wawili hawa walitajwa kuwa mapenzini kitambo na hata
ujauzito wa Aunty iliandikwa kwamba baba kijacho ni Mose japo Aunty mwenyewe
alikanusha.
Nakumbuka alisema ‘kuhusu taarifa za mimi kupewa ujauzito na
Mose Iyobo, hizo taarifa mwenyewe nasoma kwenye magazeti nasikia kwenye Radio
kama unavyosema lakini mimi binafsi ndio najua hii mimba ni ya nani‘
Pamoja na kukanusha huko, wawili hawa wameendelea kuchukua
nafasi kwenye vichwa vya habari kutokana na post zao wenyewe kwenye page za
instagram wanazomiliki ambapo wiki mbili zilizopita Mose aliweka hii picha hapa
chini huku Aunty akiwa juu yake kitandani na kuandika ‘Nzi kufa kwenye kidonda
sio ufala ila……..?
Aunty ambae ni mjamzito kwa sasa akiwa na Mose Iyobo.
Kingine kilichokolezea imani za wengi kwamba wawili hawa
wapo mapenzini kweli ni Post ya Aunty Ezekiel siku ya Valentine ambapo alipost
picha ya Mose na kuandika ‘Happy Valentine Moo akee Baby akee boo boo wa mm
baba akee………. Jaden, Baba wa…………… Umbea tyuuuu nimemaliza waone kwanza, Aunty
akee lv u‘
Baada ya hii post ya Aunt, saa kadhaa baadae kwenye siku ya
Wapendanao Mose alikolezea tena kwa kupost picha ya Aunty na mtoto na kuandika
‘Kabla siku haijaisha hawa ndio washikaji zang…… THEY JUST SAY MY DAD IS THE
BEST’
No comments:
Post a Comment