Watu watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa akiwemo dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na kupinduka na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro Dar es Salaam.
Mwandishi wetu alishuhudia kikosi cha zimamoto ambao walichukua muda kuuzima moto huo kutokana na kusambaa ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya watu kujitokeza kuiba mafuta kama ilivyozoeleka.
Baada ya kumaliza kuuzima moto huo kikosi cha zimamoto na uokoaji wakafanya juhudi nyingine za kuvuta kwa craine na kukata kwa kutumia mashoka mabaki ya lori hilo baada ya walioshuhudia tukio hilo kueleza kuwa watu wote waliokuwemo katika gari hawakutoka ambapo baada ya muda miili mitatu iliokolewa ikiwa imeungua kabisa.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo madereva wa malori ambapo
walikuwa wakisafirisha mafuta katika kampuni moja Farhan Yusufu amesema
lori hilo lilikua limesheheni mafuta ya Dezel mali ya kampuni ya Petrol
Africa ilikua ikitokea Dar es salaam kwenda jijini Mwanza ambapo
ilipoteza uelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto.
Waliofariki
dunia ni Ahmed Dilie dereva na utingo wake aliyefahamika kwa majina ya
Emela na mtu mmoja ambaye bado hajaweza kufahamika mara moja.
Nao
wananchi walioshuhudia tukio hilo wameeleza jinsi tukio lilivyotokea
ambapo wananchi wamelalamikia eneo hilo kuwa limekuwa na matukio mengi
ya ajali na hivyo kuomba serikali kuona umuhimu wa kuweka vituo vya
zimamoto katika eneo hilo kwani magari ya zimamoto yalichukua muda mrefu
kufika kwenye eneo la tukio kutokana na umbali mrefu.
Nae
afisa mkaguzi msaidizi wa kikosi cha zima moto Hamadi Dadi ameeleza
walivyopata taraari za ajali wametumia muda mrefu kufika katika eneo la
tukio ingawa wametumia muda mrefu kuzima moto huo kutokana na mafuta
yaliyokuwa yakivuja.
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na askari walionekana muda wote kwenye eneo la tukio.
No comments:
Post a Comment