Mtu na mkewe wakifanya zoezi la kukimbia
Kufanya zoezi la kukimbia kupitia kiasi kunaweza kukudhuru
vibaya afya yako kama vile kutovaa viatu wakati huo, kulingana na ripoti ya
jarida la chuo cha Marekani cha magonjwa ya moyo.
Wanasayansi waliwachunguza zaidi ya wakimbiaji 1000 na wale
wasiokimbia katika kipindi cha miaka 12.
Wale waliokuwa wakikimbia kwa kasi isiopungua ama hata
kuongezeka kwa mda wa saa mbili na nusu kwa wiki walikuwa na uwezekano mdogo
kuaga dunia wakati huo.
Lakini wale waliokimbia kwa zaidi ya saa nne kwa wiki ama
hawakufanya mazoezi kabisa walikuwa na viwango vya juu vya kuaga dunia.
Baada ya kufanya utafiti, wanasayansi waligundua kwamba watu
wanafaa kukimbia kwa kilomita nane kwa saa na kwamba ni vyema kukimbia chini ya
masaa matatu kwa wiki kwa jumla ikiwa ni saa 2 na nusu.
No comments:
Post a Comment