Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, March 14, 2015

BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA LATOA TAMKO KUHUSU UBUNGE WA ZITTO


Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, amesema kwavile Ofisi ya Bunge haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe; Ofisi yake inaendelea kumtambua kuwa ni mbunge halali ambaye anapaswa kuendelea na shughuli zake kwa mujibu wa sheria.



Dk. Kashililah alisema ikiwa CHADEMA imeamua kumvua uanachama, wanapaswa kufuata utaratibu wa kisheria, ikiwa ni pamoja na kumwandikia barua Spika wa Bunge kumjulisha uamuzi wao ili aweze kuchukua hatua nyingine za kisheria.

Katibu huyo wa Bunge alisema baada ya Spika kupata barua hiyo atamhusisha Msajili wa Vyama ili kujua kama taratibu zimefuatwa katika kufanya uamuzi huo.

"Endapo utaratibu wa kumvua uanachama Zitto Kabwe utakuwa umefuatwa basi Spika ndiye atakayeitaarifu Tume ya Uchaguzi lakini kinyume cha hapo sheria inampa nguvu Spika wa Bunge kubatilisha au kutengua uamuzi wa kumvua ubunge," alisema Dk. Kashililah

No comments:

Post a Comment